Nina uzoefu wa zaidi ya miaka mitano katika kufundisha Kiswahili, nikishughulikia vipengele vyote viwili vya Lugha na Fasihi kwa wanafunzi wa Junior Secondary School (JSS) na Senior School. Katika kipindi chote cha huduma yangu, nimefanikiwa kupanga na kusimamia mchakato wa ujifunzaji kwa ufanisi, huku nikitumia mbinu mbalimbali za ufundishaji zinazomshirikisha mwanafunzi kikamilifu.
Nina uwezo wa kuandaa mazingira bora ya kujifunzia yanayochochea ushiriki, ubunifu na fikra pevu za wanafunzi. Hutumia mbinu mbalimbali za ufundishaji, zikiwemo majadiliano, kazi za vikundi, uigizaji, matumizi ya teknolojia na tathmini endelevu ili kufanya ujifunzaji uwe wa kuvutia, wenye tija na unaokidhi mahitaji ya wanafunzi wenye uwezo tofauti. Lengo langu ni kuhakikisha kila mwanafunzi anapata maarifa, stadi na kujiamini katika matumizi ya Kiswahili.